sw_tn/isa/24/03.md

24 lines
860 B
Markdown

# Dunia itaharibiwa kabisa na kuvuliwa kabisa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atahariibu kabisa dunia na ataondoa kila kitu chenye thamani"
# Yahwe amanena neno hili
Hapa "neno" linawakilisha kile Yahwe alichosema. "Yahwe amesema angefanya"
# Dunia inakauka na kunyauka, dunia inakauka na kutokomea
Misemo hii miwili ina maana moja. "Kila kitu juu ya dunia kitakauka na kufa"
# Dunia ... ulimwengu
Zote hizi zinawakilisha kila kiitu ambacho kipo juu ya dunia.
# Dunia inachafuliwa na wakazi wake
Watu kutenda dhambi na kufanya dunia kutokubalika kwa Mungu inazungumziwa kana kwamba watu walifanya dunia kuwa chafu kimwiili. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wamechafua dunia"
# wamevunja sheria, kukiuka amri, na kuvunja agano la milele
"hawajatii sheria na amri za Mungu, na wamevunja agano la milele la Mungu"