sw_tn/isa/17/12.md

24 lines
1.0 KiB
Markdown

# Vurumai ya watu wengi, kelele hiyo kama kelele za bahari
Vurumai ni sauti kubwa sana. "Sauti ya watu wengi, ambayo ni kubwa sana kama ya bahari"
# kushuka kwa mataifa, kushuka huko kama kushuka kwa maji mengi
Majeshi ya maadui yanaonekana kuwa na nguvu sana ambayo hakuna awezaye kuwazuia. "mataifa wanakuja wakishuka kama maji mengi"
# kushuka kwa mataifa
Neno "mataifa" lina maana ya majeshi ya mataifa hayo. "kushuka kwa majeshi ya maadui"
# kama majani yaliyokufa juu ya milima kabla ya upepo ... kama majani yanavyozunguka kabla ya dhoruba
Misemo hii miwili ina maana moja. Majeshi wa maadui inaonekana kuwa na nguvu lakini Mungu atawazuia kwa urahisi na kuwafukuza mbali. "kama majani yaliyokufa juu ya milima ambayo upepo huipuliza mbali ... kama majani ambayo huzunguka na kupulizwa mbali ambapo dhoruba hukaribia"
# hii ni sehemu ya wale
Kile kinachotokea kwao inazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambayo wanarithi. "Hiki ndicho kinachotokea kwa wale"
# wanaotupora ... wanaotuibia
Neno "..tupora ...tuibia" lina maana ya Isaya na watu wa Yuda.