sw_tn/isa/14/28.md

24 lines
1.0 KiB
Markdown

# rungu iliyokupiga imevunjika
Rungu ambayo ilimpiga Filisti inawakilisha mfalme aliyetuma jeshi lake kuwashambulia. Kuvunjika inawakilisha aidha kufa au kushindwa. "mfalme aliyetuma jeshi lake dhidi yako amekufa" au "jeshi ambalo lilikushambulia limeshindwa"
# Kwa maana katika mzizi wa nyoka kutaota kifutu ... mtoto wake atakuwa nyoka mkali anayepaa
Misemo hii miwili yote ni taswira ya mtoto wa nyoka kuwa na madhara zaidi ya nyoka. Inawakilisha mrithi wa mfalme kuwa na nguvu zaidi na katili kuliko mfalme wa kwanza.
# kifutu
aina ya nyoka mwenye sumu
# nyoka mkali anayepaa
Hapa neno "kali" huenda ina maana ya kung'atwa na sumu ya nyoka, na neno "kupaa" ina maana ya kusogea kwake kwa haraka. "nyoka mwenye sumu anayesogea kwa haraka"
# mzaliwa wa kwanza wa maskini
Hii inawakilisha maskini zaidi wa watu. "Maskini zaidi wa watu" au "maskini zaidi wa watu wangu"
# Nitaua mzizi wako kwa njaa ambaye itawaua wote waliopona wa kwako
Hapa "mzizi wako" ina maana ya watu wa Filisti. "Nitawaua watu wako kwa njaa ambayo itawaua wote waliopona wa kwako"