sw_tn/isa/13/06.md

32 lines
1.3 KiB
Markdown

# Lia kwa kelele
"Paza sauti ya juu"
# siku ya Yahwe ipo karibu
Jambo ambalo linatarajia kufanyika hivi karibuni linazungumziwa kana kwamba linakuja karibu. "siku ya Yahwe itatokea hivi karibuni"
# inakuja na uhariibifu kutoka kwa Mwenyezi
Neno "inakuja" ina maana ya siku ya Yahwe. "Inakuja na uharibifu" ina maana uharibifu utatokea katika siku hiyo. "Uharibifu kutoka kwa Mwenyezi" ina maana ya kwamba Mwenyezi atawaangamiza. "katika siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawaangamiza"
# mikono yote huning'inia kwa ulegevu
Hii inaonyesha ya kwamba watu wote ni dhaifu sana na hawawezi kufanya jambo lolote.
# kila moyo huyeyuka
Watu kuwa na hofu sana inazungumzwa kana kwamba mioyo yao huyeyuka. "kila mmoja anaogopa sana"
# uchungu na maumivu utawakamata
Watu kujisikia maumivu mabaya ghafla na majonzi inazungumziwa kana kwamba maumivu na majonzi yalikuwa watu ambao huwakamata. "ghafla watahisi maumivu makubwa na uchungu"
# kama mwanamke katika uchungu
Kuwa katika uchungu inawakilisha kuzaa mtoto. "kama mwanamke anayezaa mtoto" au "kama maumivu ya mwanamke ambaye anazaa mtoto"
# nyuso zao zitawaka
Nyuso zao kuwa za moto na nyekundu inazungumziwa kana kwamba zilikuwa zikiungua. Sababu zinazowezekana za nyuso zao kuwa za moto ni 1) watu wanaogopa sana au 2) watu wanajisikia aibu au 3) watu wanalia. "nyuso zao zitakuwa za moto na nyekundu"