sw_tn/isa/11/01.md

16 lines
996 B
Markdown

# Chipukizi litachipuka kutoka kwenye kisiki cha Yese ... tawi kutoka katika mizizi yake litazaa matunda
Isaya anamzungumzia Yese na uzao wake kana kwamba walikuwa mti ambao ulikuwa umekatwa chini. Misemo hii miwili inaelezea juu ya uzao wa Yese ambaye atakuwa mfalme. "Kama vile chipukizi linavyochipuka kutoka kwenye kisiki cha mti, vile vile uzao wa Yese utakuja kuwa mfalme juu ya kinachobaki cha Israeli"
# kisiki cha Yese
Kisiki ni kile kinachobaki kwenye mti baada ya kukatwa chini. "Kisiki" cha Yese kinawakilisha kile kinachobaki katika ufalme ambao mwana wa Yese Daudi aliwahi kuwa mfalme.
# Roho wa Yahwe atatua juu yake
Kutua juu yake inawakilisha kuwa pamoja naye na kumsaidia. Neno "yake" ina maana ya yule ambaye angekuja kuwa mfalme.
# roho ya hekima ... roho ya mafunzo ... roho ya maarifa ... hofu ya Yahwe
Hapa neno "roho" ina maana ya uwezo au sifa ambayo Roho wa Yahwe angempatia. "na atasababisha kuwa na hekima na uelewa, mafunzo na uwezo, maarifa na hofu ya Yahwe"