sw_tn/isa/07/23.md

24 lines
1.1 KiB
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Isaya anaendelea kufafanua kipindi ambacho jeshi kutoka Ashuru litashambulia nchi ya Israeli.
# palipokuwa na mizabibu elfu moja ... mibigili na miiba
"kulikuwa na mizabibu 1,000". Yaani, Isaya alipoandika, kulikuwa na mashamba ya mizabibu, ambazo baadhi yao kulikuwa na mizabibu 1,000 au zaidi. Anasema ya kwamba mashamba haya ya mizabibu yatajaa mibigili na miiba"
# shekeli elfu moja za fedha
"shekeli 1,000 za fedha". Shekeli ni sarafu ya fedha yenye thamani ya mshahara wa siku 4. "sarafu 1,000 za fedha"
# mibigili na miibaa
Maneno "mibigili" na "miiba" yote ina maana ya kutokuwa na thamani, mimea ya miiba. "vichaka vya miiba" au "vichaka vya mibigili"
# kwa sababu nchi yote itakuwa mibigili na miiba
Kwa nini wawindaji watakuja katika nchi hizi inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu hakutakuwa na kitu katika nchi hizi ila mibigili, miiba, na wanyama pori"
# Watakaa mbali na vilima vyote ambavyo vililimwa kwa jembe
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watakaa mbali na vilima ambamo hapo awali ziliandaa udongo kupanda mazao"