sw_tn/isa/01/12.md

20 lines
872 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.
# ni nani ametaka kutoka kwako, kukanyaga mahakama yangu?
Neno "kukanyaga" lina maana ya kukanyaga juu ya na kuponda kwa mguu wa mtu. Mungu anatumia swali kukaripia watu wanaoishi Yuda. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "hakuna aliyekuambia kukanyanga katika uwanja wangu wa mahakama!"
# Usilete sadaka zisizo na maana
"Usiniletee zawadi zako zaidi zisizo na maana"
# ubani ni chukizo kwangu
Hapa nomino dhahania ya "chukizo" inaweza kuelezwa kama kitenzi "chuki". "Ninachukia ubani makuhani wanayochoma"
# siwezi kustahimili mikusanyiko hii ya kiovu
Maana zawezekana kuwa 1) "Siwezi kuwaruhusu kukusanyika pamoja kwa sababu ya mambo maovu mnayofanya" au 2) "Siwezi kujiruhusu kuwatazama mkikusanyika pamoja kwa sababu ya mambo maovu mnayofanya"