sw_tn/isa/01/07.md

40 lines
1.4 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.
# Nchi yako imeharibiwa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Wameharibu nchi yako" au "Adui zako wameharibu nchi yako"
# Miji yako imeungua
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wameunguza miji yenu"
# mashamba yenu - mbele yenu, wageni wanaingamiza
"watu ambao si wa nchi yenu wenyewe wanaiba mazao kutoka kwenye mashamba yenu huku mkitazama"
# uharibifu uliotelekezwa
"tupu na kuharibiwa". Msemo huu wa nomino dhahania unaweza kuelezwa kama misemo ya kitenzi. "wameangamiza nchi na hakuna mtu anayeishi pale"
# kupinduliwa na wageni
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wageni wamepindua nchi yako" au "jeshi la kigeni limeitwaa kabisa"
# binti Sayuni amabaki
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nimemuacha binti wa Sayuni"
# binti Sayuni
"binti" wa mji ina maana ya watu wa mji. "Watu wa Sayuni" au "Watu wanaoishi Sayuni"
# ameachwa kama kibanda cha shamba la mizabibu, kama kivuli katika bustani ya matango
Maana zawezekana kuwa 1) "amekuwa mdogo kama kibanda katika shamba la mizabibu au kivuli katika bustani ya matango" au 2) "ameachwa kwa mtindo ambao mkulima huacha kibanda katika shamba la mizabibu au kivuli katika bustani ya matango anapokuwa kamalizana nayo"
# kama ... matango, kama mji uliozingirwa
Maana nyingine yaweza kuwa "kama ... matango. Yeye ni mji uliozingirwa"