sw_tn/heb/06/19.md

1.1 KiB

Sentensi Unganishi:

Baada ya kumaliza onyo lake la tatu na maneno ya kuwatia moyo waumini, mwandishi wa Waebrania anaendeleza ulinganifu wake wa Yesu kama kuhani dhidi ya kuhani Melikizedeki.

kama nanga salama na tegemewa ya roho zetu

Kama vile nanga inanyoshikilia mtumwi kutoenda sehemu nyingine ndani ya maji, Yesu anatuweka sisi sehemu salama katika uwepo wa Mungu.

ujasiri uingiao sehemu ya ndani nyuma ya pazia

Ujasiri unaongelewa kana kwamba ni mtu ambaye angeweza kwenda katika mahali patakatifu pa patakatifu pa hekalu.

sehemu ya ndani

Hii ilikuwa ni sehemu ya ndani ya hekalu.Ilidhaniwa kuwa ndiyo sehemu Mungu alikuwa akikaa miongoni mwa watu wake. Katika sura hii sehemu hii inasimama kama mbingu na chumba cha kiti cha enzi cha Mungu.

kama mtangulizi wetu

Ukweli kwamba Yesu alikufa na kufufuka, na kwamba sasa yuko na Mungu Baba, inaonyesha kwamba sisi tunaoamini katika yeye tutapata mambo yaleyale.Yesu anaoglewa hapa kana kwamba ni mtu ambaye anakimbia mbele yetu na kwamba tunamfuata.

kwa mfano wa Melikezedeki

Hii ina maana kuwa Kristo kama kuhani ana vigezi sawa na vya kuhani Melikizedeki,