sw_tn/heb/04/12.md

48 lines
1.9 KiB
Markdown

# neno la Mungu li hai
"Neno la Mungu" hapa linamaanisha kila kitu ambacho Mungu ameongea kwa wanadamu iwe kwa kuongea au kwa kupitia ujumbe ulioandikwa.
# lina hai na lina nguvu
Hii inaongelea neno la Mungu kana kwamba linaishi. Inamaanisha wakati Mungu anapoongea ni kuna nguvu na utendaji kazi.
# lina ukali kuliko upanga wowote wenye makali mawili
upanga wenye makali. upanga wenye makali kuwili ni rahisi kukata kupitia mwili wa mtu. Neno la Mungu lina nguvu katika kuonyesha kilichomo katika moyo na mawazo ya watu.
# Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho.
Hii inaendelea kuongea kuhusu neno la Mungu kana kwamba ulikuwa ni upanga. Upanga hapa ni mkali sana kiasi kwamba unaweza kukata na kugawa viungo vya mwanadamu ambavyo ni vigumu pengine visivyo wezekana kugawanyika.
# nafsi na roho
Haya ni maneno mawili tofauti lakini sehemu za mwanadamu ambazo hazina mwili. "Nafsi" ndiyo inamfanya mtu kuwa hai na "roho" ni sehemu ya mtu ambayo inamsababisha kuweza kumjua na kumwamini Mungu.
# viungo kutoka maboho
"kiungo" ndicho kinacho shikilia mifupa miwili pamoja. "uboho" ni sehemu ya kati ya mfupa.
# kuweza kufahamu
Hii inaongea neno la Mungu kana kwamba ni mtu ambaye angewezakujua kitu.
# mawazo na makusudi ya moyo
Hii inaongea kuhusu moyo kana kwamba ni sehemu ya kati ya mawaazo na hisia za mwanadamu.
# Hakuna kilichoumbwa kilichojificha katika uso wa Mungu
Hili linaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. AT: "hakuna kitu kilichoumbwa na Mungu kinaweza kujificha mbele zake"
# kila kitu kiko wazi
Hii inaongelea kila kitu kana kwamba ni mtu amesimama wazi au boksi lililo wazi.
# wazi na iliyo wazi
Kimsingi maneno haya mawilii yanamaanisha kitu kimoja na kusisitiza kwamba hakuna kitu chochote kilichojificha mbele za Mungu.
# kwa macho ya yule tutakaye toa hesabu
Mungu anaongelwa kana mwamba ana macho ya nyama. AT" Mungu atatuhukumu kulingana na vile tulivyoishi"