sw_tn/heb/04/01.md

24 lines
1.3 KiB
Markdown

# Sentensi Unganishi
Sura ya 4inaendeleza onyo lililoanza katika sura ya 3:7.Mungu kwa kupitia mwandishi anawapa waumini pumziko ambalo pumziko la Mungu katika uumbaji dunia ni picha.
# kati yenu asiwepo hata mmoja atakayeweza kuonekana kushindwa kuifikia ahadi ya kuingia katika pumziko la Mungu iliyobaki kwa ajili yenu
Ahadi ya Mungu inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni zawadi iliyoachwa baada ya Mungu kuwatembelea watu. AT: "mmoja wenu asishindwe kuingia katika pumziko la Mungu , ambalo alituahidi".
# kuingia katika pumziko la Mungu
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu huongelewa kana kwamba vilikuwa ni pumziko ambalo anaweza kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. AT: "kuingia katika sehemu ya pumziko" au "kupata baraka za pumziko la Mungu.
# Kwani tumekuwa na habari njema kama walivyokuwa nazo
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Kwa kuwa tulisikia habari njema kama walivyosikia"
# kama walivyo
walivyo hapa linamaanisha mababu/mababa wa Kiebrania ambao walikuwa hai wakati wa Musa.
# Lakini ujumbe ule haukuwafaa wale ambao hawakuungana katika imani pamoja na wale walio tii
"Lakini ujumbe ule haukuwafaa wale ambao hawakuungana na watu walio amini na kutii." Mwandishi anaongea kuhusu makundi mawili ya watu, wale waliopokea agano la Mungu kwa imani, na wale walio sikia lakini hawakuamini.