sw_tn/gen/48/03.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown

# Luzu
Hili ni jina la mji.
# katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na kuniambia
Hii inaweza kutafsiriwa kwa sentensi mpya ikianzia katika sehemu mpya. "katika nchi ya Kaanani, na akanibariki. Na akasema kwangu"
# akanibariki
Hii ina maana ya Mungu kutamka baraka rasmi kwa mtu.
# na kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele
Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "na kusema kwangu ya kwamba angenifanya niwe na uzao mwingi na kunizidishia. Na akasema ya kwamba angenifanya kuwa kusanyiko la mataifa na angenipa nchi hii kwa uzao wangu kama milki ya milele".
# Tazama
Mungu alitumia neno hili "tazama" hapa kumuamsha Yakobo kuvuta nadhari kwa kile alichokuwa akitaka kumwambia.
# nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha
Msemo "kukuzidishia" unaelezea jinsi ambavyo Mungu angemfanya Yakobo "kupata uzao". "Nitakupatia uzao mwingi sana"
# Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa
Hapa "nitakufanya" ina maana ya Yakobo, lakini ina maana ya uzao wa Yakobo. "Nitafanya vizazi vyako kuwa mataifa mengi"
# milki ya milele
"milki ya kudumu"