sw_tn/gen/41/30.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Yusufu anaendelea tafsiri ya ndoto za Farao.
# miaka saba ya njaa itakuja baada yake
Hii inazungumzia kuhusu miaka saba ya njaa kana kwamba miaka ni kitu kinachosafiri na kufika mahali. "Kisha kutakuwa na miaka saba ambayo kutakuwa na chakula kichache"
# wingi wote katika nchi ya Misri utasahaulika ... na njaa itaiaribu nchi. Wingi hautakumbukwa ... kwa sababu ya njaa itakayofuata
Yusufu anaonyesha wazo kwa njia mbili kusisitiza umuhimu wake.
# wingi wote katika nchi ya Misri utasahaulika
Hapa "nchi" ina maana ya watu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu wa Misri watasahau kuhusu miaka saba ambayo kulikuwa na chakula kingi"
# itaiaribu nchi.
Hapa "nchi" ina maana ya udongo, watu, na nchi nzima.
# kwa sababu ya njaa itakayofuata
Hii inazungumzia kuhusu njaa kana kwamba ilikuwa kitu kinachosafiri na kufuata nyuma ya kitu kingine. "kwa sababu ya muda wa njaa utakaotokea hapo baadae"
# Kwamba ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alikupatia ndoto mbili kukuonyesha ya kwamba hakika atasababisha mambo haya kutokea"