sw_tn/gen/19/16.md

36 lines
1.1 KiB
Markdown

# Lakini akakawia-kawia
"Lakini Lutu alisita" au "Lakini Lutu hakuanza kuondoka"
# Kwa hiyo watu wale wakamshika
"kwa hiyo wanamume wawili walimkamata" au "Kwa hiyo malaika walimkamata"
# alimhurumia
"akawa na huruma kwa Lutu". Yahwe anaelezwa kama kuwa na "huruma" kwa sababu alikuwa akitunza uhai wa Lutu na familia yake badala ya kuwaangamiza alipoangamiza watu wa Sodoma kwa maovu waliofanya.
# Walipowatoa nje
"Wanamume wawili walipowatoa familia ya Lutu nje"
# jiponye nafsi yako!
Hii ilikuwa namna ya kuwaambia wakimbie ili wasife. "Kimbia na uokoe maisha yenu!"
# usitazame nyuma
Msemo "katika mji" unaeleweka. "Usitazame nyuma katika mji" au "Usitazame nyuma katika Sodoma"
# kwenye hili bonde
Hii ina maana bonde la Mto Yordani. Hii ina maana ya jumla ya eneo la Mto Yordani.
# usije ukatoweshwa mbali
Inaeleweka ya kwamba watatoweshwa pamoja na watu wa mji. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "la sivyo Mungu atawaangamiza pamoja na watu wa mji"
# ukatoweshwa mbali
Mungu kuwaangamiza watu wa mji inazungumziwa kana kwamba mtu anafagia vumbi.