sw_tn/gen/02/04.md

40 lines
1.2 KiB
Markdown

# Taarifa ya jumla
Sura ya pili iliyobaki ya Mwanzo inaelezea juu ya Mungu alivyoumba watu katika siku ya sita.
# Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi
"Hii ni habari ya mbingu na nchi" au "Hii ni simulizi ya mbingu na nchi" Yawezekana maana ni 1) ni kifupisho cha matukio yaliyoelezwa katika Mwanzo 1:1-2:3 au 2) inakaribisha matukio yaliyoelezwa katika Mwanzo 2.
# vilipoumbwa
Yahwe Mungu aliviumba". Katika sura ya 1 mwandishi kila mara anamzungumzia Mungu kama "Mungu", lakini katika sura ya 2 kila mara anamzungumzia Mungu kama "Yahwe Mungu".
# katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba
"Yahwe Mungu alipoumba". neno "siku" linamaana ya muda wote wa uumbaji na siyo siku hiyo moja pekee.
# Yahwe
Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.
# Hapakuwa na msitu wa shambani
hapakuwa na vichaka vimeavyo msituni ambayo wanyama wangeweza kula
# hapakuwa na mmea wa shambani
hapakuwa na mimea ya majani kama mboga au mboga za kijani ambazo wanyama na binadamu wangeweza kula
# kulima
kufanya kila kitu alichopaswa kufanya ili kwamba mimea iweze kuota vizuri
# ukungu
Yawezekana maana yake ni 1) kitu kama umande au ukungu wa asubuhi au 2) chemichemi kutoka mikondo chini ya ardhi.
# uso wote wa ardhi
dunia nzima