sw_tn/gen/01/09.md

24 lines
856 B
Markdown

# Maji yaliyo chini ..yakusanyike
Hii inaweza kutafsiriwa kama kitenzi endelevu. Hii ni amri. Kwa kuamuru maji yakusanyike, Mungu aliyafanya yakusanyike pamoja.
# na ardhi kavu ionekane
Maji yalikuwa yamefunika ardhi. Basi maji yalisogea pembeni na baadhi ya ardhi kubaki wazi. Hii ni amri. Kwa kuamuru kwamba ardhi kavu ionekane, Mungu alifanya ionekane. "na ardhi kavu ionekane" au "na ardhi kavu iwe wazi" au "na ardhi ifunuliwe"
# ardhi kavu
Hii inamaanisha ardhi ambayo haijafunikwa kwa maji. Haimaanishi ardhi ambayo ni kavu sana kwa ajili ya kilimo.
# ikawa hivyo
"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.
# nchi
"ardhi" au "chini"
# Akaona kuwa ni vyema
Hapa "ni" inamaanisha nchi na bahari.