sw_tn/gal/06/11.md

1.3 KiB

Sentensi kiunganishi

Paulo akikaribia kufunga waraka wake, anawakumbusha jambo moja zaidi kwamba sheria haiokoi na kwamba wanatakiwa kuumbuka msalaba wa Yesu

barua kubwa

Hii inaweza kumaanisha kwamba Paulo anasisitiza 1)maelezo yanayofuata au 2) kwamba barua hii ilitoka kwake.

kwa mkono wangu

Maana zinazokubalika 1)Huenda Paulo alikuwa na msaidizi ambaye aliandika mambo mengi katika barua hii kama vile Paulo alimwambia kuandika, lakini Paulo mwenyewe aliandika sehemu hii ya mwisho ya barua au 2) Paulo aliandika barua hii yote yeye mwenyewe.

kufanya mema kwa kuwashawishi

"kuwafanya wengine wawafikirie vizuri" au kuwafany wengine wafikiri kuwa wao ni watu wazuri"

katika mwili

"kwa ushahidi wa kuonekana" au " kwa juhudi zao"

kulazimisha

"kushurutisha" au kushawishi kwa nguvu"

Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo

"ili kwamba Wayahudi wasiwatese kwa kusema kuwa msalaba wa Kristo pekee huokoa watu"

msalaba

Msalaba hapa unawakilisha kile ambacho Kristo alifanya kwa ajili yetu alipokufa pale msalabani. "Kazi aliyoifanya juu ya msalaba" au " kifo na ufufuo wa Yesu"

wanataka

"watu wale wanaowataka nyie mtahiriwe"

ili waweze kujivunia miili yenu

"ili kwamba wajivune kwa kuwa watakuwa wamewaongeza kwa watu wale wanaoshika sheria."