sw_tn/gal/04/08.md

855 B

Sentense unganishi

Paulo anawakumbusha tena wasomaji wake kuwa wanajaribu tena kuishi chini ya sheria badala ya kuishi kwa imani.

Maelezo ya jumla

Hapa Paulo anaendelea kuwakemea Wagalatia kwa kuwauliza maswali ya kejeli, yasiyohitaji majibu

Mnajulikana na Mungu

inaweza pia kuelezwa kwa muundo tendaji kama "Mungu anawajua"

kwa nini mnarejea tena... kanuni?

Hili swali la kwanza kati ya maswali mawili yanayo na majibu ndani yake. "Kuwa msirejee tena nyuma katika kanuni za awali."

Kanuni za awali

Maana zinazokubalika ni 1) inarejelea sheria na kanuni za kimaadili za ulimwengu 2) inarejelea nguvu za kiroho, ambazo baadhi ya watu wanadhani zinatawala kile kinachotokea duniani.

Mnataka kuwa watumwa tena?

Swali hili laweza kutafsiriwa kama maelezo tu "Hamtakiwi kuw mtumwa tena" au "Inaonyesha kuwa mnataka kuwa watumwa tena."