sw_tn/gal/04/06.md

1.3 KiB

ninyi ni wana.....si watumwa tne bali wana

Hapa Paulo anatumia neno la watoto wa kiume kwasababu ya jambo la Urithi.katika utamaduni wa wasomaji wake, urithi mara nyingi, lakini si mara zote, ulikuwa ni wa watoto wa kiume tu. Paulo alikuwa hapendelei watoto wa kiume na kuwatenga watoto wa kike hapa.

Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, "Abba, Baba."

Mungu Baba amemtuma Roho wa Mwana wa Mungu katika mioyo ya waumini. Sasa wanajua kuwa anawapenda wakati wote kama baba mwema anavyowapenda watoto wake.

Kutumwa kwa Roho wa Mwanawe ndani ya mioyo yetu.

Neno moyo limetumika kuwakilisha sehemu ya mtu inayofikiria na kuhisi. "kutuma Roho ya Mwana wake kutuonyesha jinsi ya kufikiri na kutenda"

Mwana

Hiki ni jina muhimu la Yesu, Mwana wa Mungu.

Anayeita

Roho ndiye anayeita

Abba, baba

Hii ni namna ya mtoto anavyojieleza kwa baba yake katika lugha aliyokuwa akiitumia Paulo, ingawa si katika lugha iliyokuwa ikitumiwa na wasomaji wa Galatia. Ili kutunza lugha hiyo ngeni ni vema kulitafasiri kama linavyosikika kama "Abba" ikiwa lugha yako inavyoruhusu.

wewe si mtumwa tena bali ni mwana

Paulo anawazungumzia wasomaji wake kana kwamba ni mtu mmoja, 'wewe' huu ni umoja.

warithi

Watu ambao Mungu amewapa ahadi wanaongelewa kama warithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia