sw_tn/gal/01/11.md

822 B

Sentensi Unganishi

Paulo anaeleza kuwa hakujifunza injili kutoka kwa wengine; alijifunza kutoka kwa Yesu Kristo.

Ndugu

Hapa inamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.

haitokani na watu (si injili ya watu)

kwa kutumia maneno haya, Paulo hasemi kuwa Yesu Kristo mwenyewe si mwanadamu. kwa sababu Kristo ni mtu na ni Mungu, ingawa Yeye si mwanadamu mwenye dhambi. Paulo anaandika juu ya kule injili ilikotoka, kwamba haikutoka kwa watu wenye dhambi, bali ilitoka kwa Yesu Kristo.

kilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu

Maana zinazokubalika ni 1) Yesu Kristo mwenyewe aliifunua injili kwangu 2)Mungu alinifanya mimi niijue injili wakati aliponionesha jinsi Yesu Kristo alivyo.