sw_tn/ezk/01/27.md

1.2 KiB

Maelezo ya Jumla:

Ezekieli anaendelea kueleza kuhusu maono.

kutoka kwenye nyonga juu

Mwili wa mwanadamu juu ya nyonga palifanana kama chuma kinachong'aa kilichokuwa na moto ndani mwake.

kuzunguka kote

"kuzunguka kote mtu aliyeketi juu ya kiti cha enzi"

kutoka kwenye nyonga kwa chini palionekana kama moto na mng'ao ulozunguka kote

"Kumzunguka kote chini ya nyonga, niliona kilichofanana kama moto na mwanga ung'aao."

Ilionekana kama upinde wa mvua unaoonekana katika mawingu katika siku ya mvua, na kama mwanga unaong'aa ukiizunguka

"Mwanga ambao ulikuwa umemzunguka kote ulifanana kama upinde wa mvua uonekanao katika mawingu katika siku ya mvua inyeshapo."

upinde wa mvua

rangi nzuri ya mustari wa mwanga uonekanao katika mvua wakati jua liwakapo kutoka nyuma ya mwonekano

Huu ulionekana kama mfanano wa utukufu wa Yahwe

"Mwanga unaong'aa ulifanana kama kitu ambacho kilichofanana na utukufu wa Yahwe."

niliusikia kwenye uso wangu

"nilisujudu hata chini kwenye nchi" Ezekieli hakuanguka kwa ajali. Alienda chini hata kwenye nchi kuonyesha kwamba aliheshimu na kumwogopa Yahwe.

nilisikia sauti ikinena

Neno "sauti" ni picha ya mtu. "nikasikia sauti ikinena"