sw_tn/eph/04/28.md

785 B

Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu

"msiruhusu lugha mbaya itoke kinywani mwenu" au "msiruhusu mazungumzo maovu yatoke kinywani mwenu"

Badala yake maneno ambayo ni msaada kwa kuwajenga wengine

"badala yake neneni maneno ambayo ni msaada katika kutoa afya kwa waamini wengien"

Kuwapa neema wao ambao wanasikiliza

"kwa njia hii mtatoa neema kwa wale ambao wanasikiliza"

faida

"saidia" au "msaada"

Msimhuzunishe

"msitese" au "msiudhi"

Kwa yeye ambaye mmewekewa mhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi

Paulo anasema Roho Mtakatifu amewaakikishia waamini kuwa Mungu atawapatia ahadi aliyo waahidi. Roho ni kama alama ambayo Mungu amewaekea watu wake kuonyesha kuwa anawamiliki. "Ni Roho ambaye Mungu amekupa kuonyesha kuwa anakumiliki na ata kukomboa kwa wakati muafaka"