sw_tn/eph/04/17.md

1.1 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo anawaambia wao kile ambacho hawapaswi kufanya sasa tu kwasababu wao kama waamini wamewekewa mhuri na Roho Mtakatifu wa Mungu.

Hivi nasema kwahiyo, na ninawasihi ninyi katika Bwana

"Kwahiyo, ninawatia moyo kwa nguvu katika Bwana"

Msitembee tena kama wamataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao

"Acheni kuishi kama wamataifa na fikra zao zisizonamaana"

Kutiwa giza katika fikra

Hawawezi kufikiri au kuhoji kwa usahihi.

kufukuzwa kutoka katika maisha ya Mungu kwa ujinga uliomo ndani yao na kwa ugumu wa mioyo yao

"Hawawezi kuhisi maisha ya Mungu kwa sababu akili zao zimepofushwa na ni wagumu"

Kufukuzwa

"kukatiliwa mbali" au "kutengwanisha"

ujinga

"ukosefu wa maarifa" au "ukosefu wa taarifa"

sababu ya ugumu wa mioyo yao

Wamekataa kumsikiliza Mungu na kufuata mafundisho yake.

wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu

Paulo anawaongelea awa watu kama wao ni vitu wanaojikabidhi wao wenyewe kwa watu, na anaongelea jinsi wanavyo taka kuridhisha tamaa zao za mwili kana kwamba ndio mtu wanao jikabidhi kwake. "Wanacho taka tu nikuridhisha tamaa zao za mwili"

jikabidhi

"kujitoa kabisa"