sw_tn/eph/02/19.md

1.2 KiB

ninyi watu wa mataifa si wageni na wasafiri tena. bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe wa nyumbani mwa Mungu.

Hii inaelezea hali ya kiroho ya watu wa mataifa kabla na baada ya kuwa waamini kwa namna ile ile ambayo watu wasiokuwa raia wanavyoweza kuwa raia wa taifa fulani.

si wageni tena

" si watu wa nje tena"

na wasafiri

"na watu wasio raia"

mmejengwa juu ya msingi

Paulo analinganisha Familia ya Mungu na jengo. Yesu akiwa jiwe kuu la pembeni, na mitume wakiwa ndiyo msingi na waamini wakiwa boma (jengo lenyewe)

jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukuwa kama hekalu.

Paulo anaendelea kulinganisha Familia ya Kristo na jengo. Kwa namna ile ile ambayo mjenzi anaungamanisha mawe pamoja wakati akijenga, vivyo hivyo Kristo anatuungamanisha pamoja.

ndani yake...ndani ya Bwana

Haya ni maelezo ya mfano juu ya "ndani ya Kristo Yesu". Haya yanatokea mara nyingi katika nyaraka (barua) za Agano Jipya. Yanaelezea uhusiano wa nguvu sana unaoweza kuwepo baina ya Kristo na wale wanaomwamini yeye.

ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho

Hii inaeleza namna waamini wanawekwa pamoja kuwa mahali ambapo Mungu ataishi siku zote kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu