sw_tn/eph/02/04.md

1.2 KiB

Mungu ni mwingi wa rehema

"Mungu amejaa rehema" au "Mungu ni mwema sana kwetu"

kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi

"kwa sababu ya pendo lake kubwa kwetu" au "kwa sababu anatupenda sana"

wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya

Hii inaonyesha ni jinsi gani mtu mwenye dhambi hawezi kumtii Mungu mpaka pale anapopewa maisha mapya ya kiroho kama tu vile mtu mfu asivyoweza kujishughulisha na maisha ya mwili huu isipokuwa amefufuliwa kutoka katika wafu.

alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo

"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweze kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.

alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo Yesu.

Kama alivyokwisha kumfufua Kristo, atatufufua na sisi na tutakuwa na Kristo mbinguni.

ndani ya Kristo Yesu

"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.

katika nyakati zijazo

"huko baadaye"