sw_tn/eph/02/01.md

36 lines
1.0 KiB
Markdown

# Sentensi Unganishi:
Paulo anawakumbusha waamini walivyokuwa hapa mwanzo na sasa namna walivyo mbele za Mungu.
# Na ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu
Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wana dhambi kiasi cha kushindwa kumtii Mungu kwa namna ile ile wafu wasivyoweza kujishughulisha kimwili tena.
# makosa na dhambi zenu
Maneno "makosa" na "dhambi" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Paulo anayatumia yote pamoja kuweka mkazo wa ukubwa wa dhambi ya watu.
# hapo mwanzo mlienenda
Hii inaelezea tabia ya namna watu walivyoishi
# kwa kumfuata mtawala wa mamlaka ya anga
Mtume Paulo anatumia neno "anga" kumaanisha tabia za ubinafsi na ufisadi wa watu waaishio humu duniani.
# mtawala wa mamlaka ya anga
Hii inamaanisha ibilisi au shetani
# roho yake yule
Sentensi "roho yake yule" inamaanisha ibilisi au shetani.
# Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu, tulikuwa tukifanya mapenzi mwili na ya akili.
Maneno "mwili" na "nia" yanawakilisha mwili wote.
# wana wa ghadhabu
Watu ambao Mungu amewakasirikia