sw_tn/deu/33/29.md

1.1 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" na "zako" hapa ni katika umoja.

Nani kama wewe, watu waliokombolewa na Yahwe ... utukufu?

Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. Linaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Hakuna kundi la watu wengine kama wewe ... utukufu"

ngao ...upanga

Lugha hii ya kujumlisha inamzungumzia Yahwe kuwatetea Waisraeli kutoka kwa adui zao na kuwawezesha kushambulia adui zao.

ngao ya msaada wako

Neno "ngao" ni sitiari ya Yahwe kulinda na kuteteta Waisraeli. Nomino inayojitegemea "msaada" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "yule ambaye anakulinda na kukusaidia"

upanga wa utukufu wako

Neno "upanga" ni sitiari kwa ajili ya nguvu ya kuua kwa upanga ili kushinda vita. "yule ambaye anakuwezesha kushinda vita na kuwa na utukufu"

utakanyanga sehemu zao zilizoinuka

Maana zaweza kuwa 1) Waisraeli wataangamiza sehemu ambazo watu wengine wanaabudu miungu ya uongo au 2) Waisraeli watatembea juu ya migongo ya adui zao Waisraeli watakapowashinda.