sw_tn/deu/33/21.md

468 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kubariki kabila za Israeli; baraka ni shairi fupi. Anaendelea kuelezea kabila la Gadi kama mtu mmoja, ambalo alianza kufanya katika 33:20.

fungu la kiongozi

Hii ina maana ya kipande kikubwa cha ardhi ambacho kiongozi mara nyingi alichukua.

Alikuja na vichwa vya watu

"Walikutana na viongozi wote wa Waisraeli"

Alitekeleza haki ya Yahwe na maagizo yake pamoja na Israeli

"Walitii yote ambayo Yahwe aliwaamuru Waisraeli"