sw_tn/deu/33/18.md

1.1 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kubariki kila kabila la Israeli; baraka ni shairi fupi. Anazungumza na kabila za Zabuloni na Isakari kana kwamba wao ni mtu mmoja, kwa hiyo neno "kwako" na "yako" na amri "furahi" hapa ni katika umoja.

Furahi, Zabuloni, katika kutoka kwako, na wewe, Isakari, katika mahema yako

Watu wa Zabuloni walikuwa karibu na bahari kuu. Walisafiri kwa bahari na kufanya biashara na watu wengine. Watu wa Isakari walipendelea kuishi kwa amnai na kulima ardhi na kufuga mifugo. Unaweza kufanya wazi taarifa inayoeleweka.

Huko watatoa

"Ni huko ambako watatoa"

sadaka za utakatifu

"sadaka zinazokubalika" au "sadaka zinazofaa"

Maana watanyonya wingi wa bahari, na mchanga wa ufukweni

Maana zaweza kuwa 1) watafanya biashara na watu kutoka upande wa pili wa bahari au 2) walianza kutumia mchanga kutengeneza ufinyanzi"

Maana watanyonya wingi wa bahari

Neno la Kiebrania linalotafsiriwa "kunyonya" hapa lina maana ya namna mtoto ananyonya katika ziwa la mama yake. Ina maana ya watu watapata utajiri kutokana na bahari kama mtoto anavyopata maziwa kutoka kwa mama yake"