sw_tn/deu/33/16.md

1000 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kubariki kabila za Israeli; baraka ni shairi fupi. Anaendelea kuelezea kabila la Yusufu, ambalo alianza kufanya katika 33:13.

Nchi yake ibarikiwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Na Yahwe abariki mkono wake"

wingi wake

Nomino inayojitegemea "wingi" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "kile inachotoa kwa idadi kubwa"

yule aliyekuwa kichakani

Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Yahwe, ambaye alizungumza na Musa kutoka katika kichaka kiwakacho moto"

Baraka na ifike juu ya kichwa cha Yusufu

Sitiari hii ni ya mtu anayeweka mkono wake juu ya kichwa cha mwana na kumuomba Mungu kumbariki mwana huyo. Mtu huyo hapa ni Yahwe. "Yahwe ambariki Yusufu kama baba anavyombariki mwanawe"

ifike juu ya kichwa cha Yusufu, na juu ya kichwa cha yule

Hapa "kichwa" na "juu ya kichwa" ina maana ya mtu mzima na inalenga uzao wa Yusufu. "iwe juu ya uzao wa Yusufu"

juu ya kichwa

Maana nyingine yaweza kuwa "nyusi" au "kipaji cha uso"