sw_tn/deu/32/37.md

805 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli.

wako wapi miungu yao, mwamba ambao wamekimbilia?

Yahwe anakaripia watu wa Israeli kwa kutafuta ulinzi kutoka kwa miungu mingine. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Tazama, miungu ambayo Waisraeli walifikiri ingewalinda haijaja kuwaokoa"

miungu iliyokula sadaka zao nene na kunywa mvinyo wa sadaka zao za kinywaji?

Hapa Yahwe anawadhihaki watu wa Israeli kwa kutoa sadaka kwa miungu mingine. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Miungu ambayo Waisraeli walitoa nyama na divai kwao hawajaja kuwasaidia"

Na wainuke na kukusaidia; na wawe ulinzi kwako.

Yahwe anasema hivi kuwadhihaki Waisraeli. Anajua kuwa miungu hawa hawawezi kuwasaidia. "Sanamu hizi hata hawawezi kusimama na kuwasaidia au kuwalinda"