sw_tn/deu/32/32.md

826 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Anaendelea kutoa nukuu maneno ya Yahwe.

Kwa maana mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma ... vishada vyao ni vichungu

Musa analinganisha adui ambao huabudu miungu ya uongo na watu waovu wanaoishi Sodoma na Gomora na mzabibu ambayo huzaa matunda ya sumu. Hii ina maana adui zao ni waovu na watasababisha Waisraeli kufa kama Waisraeli wataanza kutenda kama watu wanavyoishi ambao wanawazunguka.

mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kwenye mashamba ya Gomorra

Mzabibu ni sitiari ya kundi la watu. Ni kana kwamba mzabibu wao ulikuwa tawi la mzabibu ambalo liliota katika shamba la Sodoma na Gomora. "wanafanya ouvu kwa njia hiyo hiyo ambayo watu walioishi Sodoma na Gomora walifanya"

vishada vyao

"vishada vyao vya mizabibu"