sw_tn/deu/32/23.md

1.4 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Anaendelea kutoa nukuu maneno ya Yahwe.

Nitarundia maafa juu yao

Yahwe anazungumzia mambo mabaya ambayo yangetokea kwa Waisraeli kana kwamba ilikuwa kitu kama uchafu ambao unaweza kurundikana juu ya Waisraeli. "Nitahakikisha ya kuwa mambo mengi mabaya yanatokea kwao"

nitafyatua mishale yangu yote kwao

Hapa Yahwe analinganisha mambo mabaya ambayo atahakikisha yanatokea kwa Waisraeli kwa mtu anavyofyatua mishale kutoka kwenye upinde. "Nitafanya kila niwezalo kufanya kuwaua"

Watapotea kwa njaa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. Nomino inayojitegemea ya "njaa" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "kuwa na njaa". "Watakuwa wadhaifu na kufa kwa sababu wana njaa"

Wata ... njaa na kumezwa kwa joto liwakalo na uharibifu mchungu

Labda maana ya "joto liwakalo" ni 1) Waisraeli watateseka kutokana na homa au 2) hali ya hewa itakuwa na joto ajabu wakati wa kiangazi na njaa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Wata ... njaa, na joto liwakalo na maafa mabaya yatawameza" au "Wata ... njaa, na watakufa kutokana na joto lichomalo na maafa mabaya"

nitatuma kwao meno ya wanyama wa mwituni, pamoja na sumu ya vitu vitambaao mavumbini

Meno na sumu ni lugha nyingine ya wanyama wanaotumia vitu hivi kuua. "Nitatuma wanyama pori kuwauma, na vitu vitambaacho mavumbini kuwauma na kuwatia sumu"