sw_tn/deu/32/09.md

1.0 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Anavyozungumza kwa Waisraeli, anaongea juu yao kana kwamba walikuwa mtu mwingine na kana kwamba walikuwa mtu mmoja.

Kwa maana fungu la Yahwe ni watu wake; Yakobo ni mgao wa urithi wake

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inaweza kuunganishwa. "Uzao wa Yakobo ni urithi wa Yahwe"

Alimpata ... alimkinga na kumtunza ... alimlinda

"Alimpata Yakobo ... alimkinga na kumtunza ... alimlinda" Unaweza kutafsiri hii kana kwamba Musa alikuwa akizungumza kuhusu Waisraeli kama watu wengi. "Aliwapata mababu zetu ... akawakinga na kuwatunza .. akawalinda"

jangwa kame na livumalo upepo

Hapa "livumalo" ina maana ya sauti ambayo upepo inafanya inapovuma katika nchi tupu.

alimlinda kama mboni ya jicho lake

Hii ni lahaja. Mboni ya jicho ina maana ya sehemu ya giza ya jicho ambayo humruhusu mtu kuona. Hii ni sehemu muhimu sana ya mwili. Hii ina maana ya kwamba watu wa Israeli ni muhimu sana kwa Mungu na kitu anachokilinda. "alimlinda kama kitu chenye thamani sana.