sw_tn/deu/31/27.md

40 lines
1.2 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Musa anaendelea kuzungumza na Walawi kuhusu watu wote wa Israeli.
# uasi wako na shingo yako ngumu
Musa anazungumza na Walawi kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "yako" ni katika umoja.
# shingo yako ngumu
"mkaidi"
# itakuaje baada ya kifo changu?
Swali hili la balagha linasisitiza jinsi watu walivyokuwa waasi. Inaweza kutafsiriwa kama kauli. "utakuwa muasi zaidi baada ya kufa kwangu"
# ili nizungumze maneno haya masikioni mwao
Hapa "masikioni mwao" ina maana ya watu wenyewe. "ili kwamba niweze kuzungumza maneno ya wimbo huu kwao"
# kuziita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yao
Maana zaweza kuwa 1) Musa anawaita wale wote wanaoishi mbinguni na duniani kushuhudia kile asemacho au 2) Musa anazungumza na mbingu na dunia kana kwamba vilikuwa binadamu, na anawaita wawe mashahidi kwa kile asemacho. Msemo kama huu unajitokeza katika 30:19
# mtajiharibu kabisa
"mtafanya kile ambacho ni kibaya kabisa"
# kugeuka kuiacha njia niliyowaamuru
"acha kufuata maagizo niliyokupatia"
# kwa sababu mtafanya yaliyo maovu machoni pa Yahwe
Hapa "machoni pa Yahwe" ina maana "kwa maoni ya Yahwe"
# kwa mikono ya kazi yenu
Hapa "mikono yako" ina maana ya watu wenyewe. "kwa sababu ya kile ulichotengeneza"