sw_tn/deu/30/01.md

1.2 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" hapa ni katika umoja.

Vitu hivi vitakavyokuja juu yako

Hapa "vitu hivi" ina maana ya baraka na laana inayoelezwa katika sura ya 28-29. Msemo "itakavyokuja juu yako" ni lahaja ambayo ina maana ya kutokea. "Vitu hivi vyote vitakavyotokea kwako"

ambazo nimeziweka mbele yako

Hii inazungumzia juu ya baraka na laana ambazo Musa aliwaambia watu kana kwamba walikuwa vyombo ambavyo aliviweka kando mbele yao. "ambayo nimekwisha kukuambia sasa hivi

utakapozirejea akilini

Hii ni lahaja. "kumbukeni"

miongoni mwa mataifa mengine

"utakapokuwa ukiishi katika mataifa mengine"

kawapeleka

"amekulazimisha kuondoka"

kutii sauti yake

Hapa "sauti" ina maana ya kile Yahwe anachosema. "tii kile anachosema"

kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote

Lahaja ya "kwa moyo .... wote" ina maana ya "yote" na "yako yot ... nafsi" ina maana "na nafsi yako yote". Misemo hii miwili ina maana moja. "kwa nafsi yako yote" au "kwa nguvu zako zote"

atageuza kutekwa kwako

"kuwaweka huru kutoka kifungoni kwako". Nomino inayojitegemea ya "kutekwa" inaweza kutafsiriwa kama kishazi. "kukuweka huru kutoka kwa yule aliyekukamata"