sw_tn/deu/26/14.md

1.0 KiB

Taarifa ya Jumla:

Hii inaendeleza kile ambacho Muisraeli anapaswa kusema kwa Yahwe anapotoa zaka yake kwa maskini.

Sijala kati yao wakati wa maombolezo yangu

"Sijala chochote katika zaka nilipokuwa nikiomboleza"

nilipokuwa mchafu

Hapa "mchafu" ina maana ya mtu ambaye sio msafi kulingana na Sheria. Mungu haruhusu mtu aliye mchafu kugusa zaka anayotoa kwa Mungu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "nilipokuwa mchafu kulingana na Sheria" au "sheria inaposema siwezi kuigusa"

Nimesikiliza sauti ya Yahwe Mungu wangu; Nimetii kila kitu ulichoniamuru kukifanya

Hapa "sauti ya Yahwe" ni lugha nyingine kwa kile Yahwe alichosema. Kauli hizi mbili zinatumia maana moja. Zinasisitiza ya kwamba mtu ametii amri zote za Mungu.

kutoka mahali patakatifu unapoishi, kutoka mbinguni

Misemo hii miwili ina maana moja. "kutoka mbinguni, sehemu yako takatifu"

nchi inayotiririka kwa maziwa na asali.

Hii ni lahaja. "nchi ambapo kuna maziwa na asali inayotiririka" au "nchi ambayo inafaa sana kwa mifugo na kilimo"