sw_tn/deu/24/17.md

849 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" hapa ni katika umoja.

Haupaswi kutumia nguvu kuchukua haki inayomhusu mgeni au yatima

Musa anazungumzia haki kana kwamba ilikuwa kitu halisi ambacho mtu mwenye nguzu zaidi anaweza kukivuta kwa nguvu kutoka kwa mtu mnyonge. "Haupaswi kumtendea mgeni au yatima kinyume na haki"

yatima

Hii ina maana ya watoto ambao wazazi wote wamefariki na hawana ndugu wa kuwatunza.

wala kuchukua vazi la mjane kama dhamana

Mkopeshaji huchukua kitu kutoka kwa mkopaji kuhakikisha ya kuwa angewez kumlipa. Hakuruhusiwa kuchukua vazi lake kwa maana alihitaji kumpatia joto. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "na usichukue vazi la mjane kama dhamana kwa sababu anahitaji kuwa na joto"

ukumbuke

Hii ni lahaja. "kumbuka"