sw_tn/deu/22/23.md

990 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza na Waisraeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "yako" hapa ni katika umoja.

amechumbiwa na mwanamume

"'ambaye ameahidiwa kuolewa na mwanamume"

wachukueni ... kuwapiga mawe

Amri hizi zinatamkwa kwa Israeli kama kundi na kwa hiyo zipo katika wingi.

wachukueni wote wawili

"kisha unapaswa kuwaleta wote msichana na mwanamume aliyelala naye"

kwa sababu hakupaza sauti

"kwa sababu hakupaza sauti kuomba msaada"

kwa sababu amemwingilia mke wa jirani yake

Katika wakati huo Waisraeli walimchukulia mwanamume na mwanamke ambao walikuwa wamechumbiana kwa ajili ya ndia kama mume na mke. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu alilala na msichana ambaye alikuwa wa Muisraeli mwenzake"

nanyi mtakuwa mmeondoa uovu miongoni mwenu

Kivumishi cha "uovu" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "unapaswa kuondoa miongoni mwa Israeli mtu ambaye anafanya jambo hili ovu" au "unapaswa kumuua mtu huyu muovu"