sw_tn/deu/21/22.md

28 lines
919 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba alikuwa akizungumza na mtu mmoja, kwa hiyo maneno "zako" na "yako" ni katika umoja.
# Iwapo mwanamume kafanya dhambi inayostahili kifo
"Iwapo mwanamume amefanya jambo baya sana hadi unahitajika kumuadhibu kwa kumuua"
# akauwawa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kumuua" au "utamuua".
# kwa kunyongwa juu ya mti
Maana zaweza kuwa 1) "na baada ya kufa unamnyonga ju ya mti" au 2) "na utamuua kwa kumyonga katika nguzo ya mbao"
# unamzika siku hiyo
"mzike katika siku hiyo hiyo ambayo umemuua"
# kwa maana yeyote anyongwaye amekwisha laaniwa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. Maana zaweza kuwa 1) "kwa sababu Mungu hulaani kila mtu ambaye watu humyonga kwenye miti" na 2) "watu huwanyonga mtini wale ambao Mungu amewalaani"
# usitie najisi nchi
kwa kukiacha kitu ambacho Mungu amekilaani kikining'inia juu ya mti.