sw_tn/deu/21/15.md

1.1 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

a mmoja wao amempenda na mwingine kamchukia

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. Maana zaweza kuwa 1) "na mwanamume anampenda mmoja wa wake zake na kumchukia mke mwingine" au 2) "na mwanamume anampenda mke mmoja zaidi ya anavyompenda mke mwingine"

na wote wamekwisha mzalia watoto

"na wake wote wawili wakapata watoto kupitia kwake"

kama mzawa wa kwanza ni wa mke asiyependwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kama mzawa wa kwanza ni wa mke ambaye mwanamume anamchukia"

basi katika siku ambayo mwanamume

"pale ambapo mwanamume"

mwanamume atakapowarithisha mali zake wanawe

"mwanamume akatoa mali yake kwa wanawe kama urithi"

hapaswi kumfanya mwana wa mke ampendaye kuwa mzawa wa kwanza kabla ya mwana wa mke amchukiaye

"hapaswi kumfanya mwana wa mke anayempenda kana kwamba alikuwa mwana wa kwanza badala ya mwana wa mke asiyempenda"

mara mbili ya sehemu

"mara mbili zaidi"

huyo mwana ni mwanzo wa nguvu zake

Hii ni lahaja. "mwana huyo ndiye anayeonyesha ya kwamba mwanamume huyo anaweza kuwa baba wa wanawe"