sw_tn/deu/20/06.md

835 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuelezea matukio yanayomruhusu mtu kuondoka jeshini.

Kuna yeyote ambaye amepanda ... Acha aende nyumbani

"Iwapo askari yeyote hapa ana shamba la mzabibu, lakini bado hajavuna matunda yake, anapaswa kurudi nyumbani kwake"

ili kwamba asife vitani na mtu mwingine afurahie matunda yake

Afisa anaelezea tukio ambalo linaweza kutokea kwa askari. "ili kwamba, kama atakufa vitani, mwanamume mwingine asivune matunda yake badala yake"

Ni mtu yupi aliyeposa kuoa mwanamke ... Acha aende nyumbani

"Iwapo askari yeyote hapa ameahidi kumuoa mwanamke, lakini bado hajamuoa, anapaswa kurudi nyumbani kwake"

ili kwamba asife vitani na mume mwingine amuoa

Afisa anaelezea tukio ambalo linaweza kutokea kwa askari. "ili kwamba, kama atakufa vitani, mwanamume mwingine asimuoe mwanamke badala yake"