sw_tn/deu/06/13.md

990 B

Taarifa ya ujumla

Musa aendelea kuwaambia watu wa Israeli maneno ya Yahwe kama wanaisraeli wako mtu mmoja.

Utamheshimu Yahwe Mungu wako; yeye utamwabudu, na utaapa kwa jina lake

"Ni Yahwe Mungu wenu na hakuna mmoja mwingine ambaye mtaheshimu; ni yeye peke yake ambaye mtamwabudu, na ni kwa jina lake na jina lake pekee mtaapa." Lugha yenu inaweza kuwa na njia nyingine ya kusisitiza kwamba Yahwe anawaambia wanaisraeli kutomwabudu au kumtumikia mungu mwingine.

utaapa kwa jina lake

Kuapa kwa jina la Yahwe ina maana kumfanya Yahwe msingi au nguvu ambayo inatumiwa kufanya kiapo. Maneno "jina lake" urejea kwa Yahwe mwenyewe.

katikati yenu

"ambaye anaishi miongoni mwenu"

hasira ya Yahwe Mungu wenu itawashwa dhidi yenu

Musa analinganisha hasira ya Yahwe na yeyote anawasha moto kuharibu vitu. Hii inaweza kutajwa kwa kauli tendaji. Kuwasha hasira ni mfano wa kuwa na hasira sana.

kuwaharibu ninyi toka

"kuwaharibu ili kwamba hakuna chochote kilichobaki kwenu popote"