sw_tn/dan/12/12.md

702 B

Maelezo ya jumla

Malaika anaendelea kuongea na Danieli.

Ana heri mtu yule anayengojea

"amebarikiwa mtu ambaye anasubiri" au "ana heri yeyote anayengojea"

anayengojea

"kuvumilia" au "kubakia mwaminifu"

siku 1,335

Mahali hapa "siku" inarejelea kipindi cha muda. Mara nyingine hueleweka kama siku, ingawa pia ina maana ya miaka.

Unapaswa uondoke

"Danieli, lazima uende" Hii inamrejelea Danieli kuendelea kuishi na kumtumikia mfalme mpaka muda uliopangwa wa kifo chake.

utapumzika

Hii ni njia ya upole ya kusema kuwa "utakufa"

Utainuka

Hii inarejelea Ufufuo wa kwanza wa wafu wakati ambao watu wenye haki watafufuliwa.

ehemu uliyopewa

"sehemu ambayo Mungu amekupatia wewe"