sw_tn/dan/11/33.md

2.0 KiB

watajikwaa

Mahali hapa " kujikwaa" inawakilisha kupatwa na majanga ya aina hii au nyingine, ikijumuisha na kifo chenyewe.

Upanga

Mahali hapa "upanga"unawakilisha mapigano na vita.

miali ya moto

Mahali hapa "miali" inawakilisha moto.

watatiwa mateka

"kufanywa kuwa mtumwa"

kunyang'anywa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Maadui zao watawaibia mali zao"

watasaidiwa kwa msaada kidogo

Hii yaweza kuwekwa katika muundo tendaji. " watu wengine watampa msaada kidogo"

Watu wengi watajiunga nao wenyewe katika unafiki

Hii inarejelea watu wengine ambao watajifanya kuwasaidia watu wenye hekima, lakini si kwasababu wamekusudia kuwasaidia kweli.

watajiunga nao

Mahali hapa "watajiunga nao" ina maana ya "kuja na kuwasaidia"

ili kujisafisha kutokee kwao,

Neno "ili" lina maana kwamba "matokeo kwamba"

Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa

Mahali hapa " kujikwaa" inawakilisha kupatwa na majanga ya aina hii au nyingine, ikijumuisha na kifo chenyewe

kujisafisha kutokee kwao, na kujiosha, na kujitakasa

Matendo haya yanaelezwa hapa kana kwamba ilikuwa ni vitu. Ingawa, yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji au tendewa. "watasafishwa, kuoshwa na kutakaswa"

kujisafisha

Hii inarejelea kusafisha kito kwa kukiyeyusha katika moto. Wakati Mungu anawatengeneza watu wake ili wawe waaminifu kwake, kunasemwa kana kwamba walikuwa ni vito ambavyo mfanyakazi alikuwa akivifanya kuwa safi zaidi kwa kuviweka katika moto.

kujiosha,

Hii inarejelea kitendo cha kuwatengeneza watu, sehemu au vitu ili vifae kwa ajili ya Mungu kwa kuvitenga na dhambi au aina nyingine yoyote ya ubaya. Uovu unasemwa kana kwamba ni uchafu wa kawaida.

kujitakasa,

Hili wazo ni sawa na kujisafisha, lililojadiliwa awali. Kito kilichosafishwa chaweza kusemwa kwamba chaweza kutakaswa.

wakati wa mwisho.

"siku za mwisho" au " mwisho wa ulimwengu.

Kwa kuwa wakati ulioamriwa haujaja bado

Mahali hapa 'wakati ulioamriwa' ina maana kwamba Mungu amepanga muda. Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Yahweh amepanga muda kwa wakati ujao"