sw_tn/dan/09/17.md

945 B

Basi sasa

Hii haina maana ya "wakati huu", bali ni njia ya kuonesha kwamba jambo jingine linalofuata katika maombi ya Danieli liko karibu kuanza.

mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema;

Maneno "mtumishi wako" na "yake" yanamrejelea Danieli. Anajiongelea yeye mwenyewe katika nafsi ya tatu kama ishara ya heshima kwa Mungu.

maombi kwa ajili ya rehema

"dua kwa ya huruma"

ufanye uso wako ung'ae

Mwandishi anamwongelea Yahweh akitenda kwa neema kana kwamba Uso wa Yahweh uling'aa kwa mwanga.

sehemu yako takatifu

Inarejelea hekalu la Yerusalemu

fungua masikio yako na usikie

"kufungua masikio yako na kusikia" ni nahau yenye maana ya kusikia. Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kile kile na kukazia hamu ya Danieli kwa Mungu ili ayasikilize maombi yake.

unaoitwa kwa jina lako

Mahali hapa "jina'' linawakilisha umiliki. "ni mali yako"

usichelewe

Hii yaweza kuelezwa kwa sentensi chanya. "fanya haraka"