sw_tn/dan/07/09.md

1.6 KiB

Maelezo ya jumla

Vifungu vingi vya mistari 9-14 ni lugha ya picha ikiwa na mistari sambamba iliyo na maana sawa.

viti vya enzi vilikuwa vimewekwa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " mtu fulani aliviweka viti vya enzi katika sehemu zake"

Mtu wa Siku za Kale

Hili jina la Mungu ambalo lina maana kwamba yeye ni wa milele.

alikaa sehemu yake...mavazi yake... nywele zake

"Kifungu hiki kinamwelezea Mungu akiwa amekaa, akiwa na mavazi na nywele kama mtu. Hii haina maana kwamba Mungu yuko hivyo, bali ni vile ambavyo Danieli alivyomwona Danieli katika maono.

alikaa sehemu yake

Hii ni lugha ya picha ikiwa na maana ya kwamba Mungu alikaa katika kiti chake cha enzi.

Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji

Mavazi yake yanalinganishwa na theruji kuonesha kwamba zilikuwa ni nyeupe sana. "nguo zake zilikuwa nyeupe sana"

ywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu

nywele za Mungu zilionekana kama sufu. maana zinazokkubalika ni 1) zilikuwa ni nyeupe sana 2) zilikuwa ni nzito na zilizopinda pinda.

sufu safi

"sufu nzuri" au "sufu zilizooh

Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto

Hii inafafanua juu ya kiti cha enzi cha Mungu na magurudumu yake kana kwamba yalikuwa yametenenezwa kwa moto. Maneo''miali ya moto' na 'kuwaka moto" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na inaweza kufasiriwa kwa namna ile ile.

magurudumu yake

Haiko wazi sana kwanini kiti cha enzi cha Mungu kinaelezwa kuwa na magurudumu. Viti vya enzi kikawaida huwa havina maguruduma, lakini kifungu kwa uwazi kinaelezea kwamba kiti hiki cha enzi kilikuwa na magurudumu.