sw_tn/dan/07/04.md

833 B

Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba

Huyu ni mnyama wa ishar, na si mnyama halisi anayeishi.

mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu

Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mtu fulani alipasua mabawa yake na kumwinua kutoka chini na kumifanya asimame kwa miguu miwili kama binadamu."

Na alipewa akili za kibinadamu

Mahali hapa neno "akili" limetumika kumaanisha "fikra.' Muundo tendaji waweza kutumika. "Mtu fulani alimpa uwezo wa kufikiri kama mtu"

kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu

Huyu hakuwa dubu halisi, bali ni mnyama wa ishara ambaye alifanana na dubu.

mbavu

Mifupa mikubwa ya kifuani iliyopinda ambayo imeungana na uti wa mgongo.

aliambiwa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mtu fulani alimwambia"