sw_tn/dan/04/34.md

613 B

Maelezo ya jumla

Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.

katika mwisho wa siku

Hii inarejelea miaka saba katika 4:31

utimamu wa akili nilirudishiwa

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "utimamu wangu ulirudi kwangu"

nilimheshimu na kumtukuza

Maneno yote yanarejelea kitendo kile kile

Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.

Virai vyote viwili vinamaanisha kimsingi kitu kile kile na vimetumika kwa kutia mkazo juu ya jinsi utawala wa Mungu usivyo na mwisho.