sw_tn/dan/03/06.md

972 B

Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto

Sentensi hii yaweza kuandikwa kwa muundo tendaji. " Wanajeshi watamtupa katika tanuru liwakalo moto mtu yeyote ambaye hataanguka na kuabudu sanamu katika muda ule watakaposikia muziki."

kuanguka

Hili ni tendo linaloonesha alama ya kuabudu.

tunuru liwakalo moto

Hiki ni chumba kikubwa kilicho jazwa moto

watu wote, mataifa na lugha

Maneno haya yanajumuisha kundi kubwa la maafisa kutoka katika miko mbalimbali waliokuwapo hapo.

sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki,

Hivi ni vyombo vya muziki.

walianguka na kuisujudia wao wenyewe

Haya ni matendo yanayoonesha ibada.

sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.

Hii inaongelea juu ya Mfalme Nebukadneza kutoa agizo kwamba ijengwe sanamu kana kwamba aliijenga mwenyewe. "Sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza aliwaagizawatu wake waiweke."